-
01
Chochote unachoweka kutangaza kupitia G-Konekti hakitakiwi kuwa na muonekano au maudhui ya kudhalilisha , kubagua wala yanayokinzana na maadili ya Kiafrika.
-
02
Tangazo lako baada ya kulipiwa halitawekwa mtandaoni moja kwa moja ,bali litafanyiwa ukaguzi {Review} ndani ya masaa 24, na kama litakidhi vigezo litawekwa mtandaoni , na kama litakuwa halijakidhi vigezo utapewa taarifa ya kutolewa.
-
03
Ukikiuka vigezo na masharti kwa kuweka picha au maudhui yeyote yasiyofaa kwenye akaunti yako utapewa adhabu ya kuzuiwa kutumia akaunti yako katika kipindi kati ya mwezi mmoja na miaka 3 na endapo baada ya adhabu ukafanya tena kosa lilelile au linalofanana na lile basi utafungiwa akaunti yako na kutoruhusiwa kutumia G-Konekti.
-
04
Endapo unapata changamoto yeyote ya utumiaji wa G-Konekti wasiliana na wahudumu wetu muda wote.
-
05
Ili kuvutia watu kuona na kununua bidhaa au huduma yako jitahidi kuweka picha zenye mvuto, zilizopigwa kwa ustadi.
-
06
Mtandao wetu wa G-Konekti hauruhusu matumizi ya lugha za matusi au lugha za kibaguzi na maudhi.
-
07
Mpendwa mtumiaji wa G-Konekti mtandao wetu ni salama sana kwa kuwakutanisha muuzaji na mnunuzi wa bidhaa /Huduma .
TAFADHARI; Jiridhishe usalama na ubora wa bidhaa/Huduma kabla ya kununua. G-Konekti haitahusika na utapeli wowote utakaofanyika baina ya muuzaji na mnunuzi nje ya mfumo wetu wa G-Konekti.
-
08
Mpendwa unaetangaza bidhaa/Huduma yako tafadhari weka taarifa sahihi za muuzaji na hali ya bidhaa au huduma . udanganyifu wowote ni kosa .
-
09
Mtandao wa G-Konekti unamilikiwa na GREDO COMPANY LTD . Hivyo utakuwa unapata taarifa mbalimbali kupitia ujumbe wa maandishi kutoka GREDO.
-
10
Mtandao wa G-Konekti umesajiliwa, ni salama na una haki miliki zote , Hivyo hupaswi kunakili chochote kwa matumizi binafsi bila ruhusa ya wamiliki.