- 
                                01
                                Chochote unachoweka kutangaza kupitia G-Konekti hakitakiwi kuwa na muonekano au maudhui ya kudhalilisha , kubagua  wala yanayokinzana na maadili ya Kiafrika.
                            
 
                            
                            - 
                                 02
                                Tangazo  lako baada ya kulipiwa halitawekwa mtandaoni  moja kwa moja ,bali litafanyiwa ukaguzi {Review} ndani ya masaa 24, na kama litakidhi vigezo litawekwa mtandaoni , na kama litakuwa halijakidhi vigezo utapewa taarifa ya kutolewa.
                            
 
                                
                            - 
                                 03
                                Ukikiuka vigezo na masharti kwa kuweka picha au maudhui yeyote yasiyofaa kwenye akaunti yako utapewa adhabu ya kuzuiwa kutumia akaunti yako katika kipindi kati ya mwezi mmoja  na miaka 3 na endapo baada ya adhabu ukafanya tena kosa lilelile au linalofanana na lile basi utafungiwa akaunti yako na kutoruhusiwa kutumia G-Konekti.
                            
 
                            
                            - 
                                 04
                                Endapo unapata changamoto yeyote ya utumiaji wa G-Konekti wasiliana na wahudumu wetu muda wote.
                            
 
                            
                            - 
                                 05
                                Ili kuvutia watu kuona na kununua bidhaa au huduma yako jitahidi kuweka picha zenye mvuto, zilizopigwa kwa ustadi.
                            
 
                            
                            - 
                                 06
                                Mtandao wetu wa G-Konekti  hauruhusu  matumizi ya lugha za matusi au lugha za kibaguzi na maudhi.
                            
 
                            
                            - 
                                 07
                                Mpendwa mtumiaji wa G-Konekti mtandao wetu ni salama sana kwa kuwakutanisha muuzaji na mnunuzi wa bidhaa /Huduma .
                                
                                    TAFADHARI; Jiridhishe  usalama na ubora wa bidhaa/Huduma kabla ya kununua. G-Konekti haitahusika na utapeli wowote utakaofanyika baina ya muuzaji na mnunuzi nje ya mfumo wetu wa G-Konekti.
                                
                             
                            
                            - 
                                 08
                                Mpendwa  unaetangaza bidhaa/Huduma yako tafadhari weka taarifa sahihi za muuzaji na hali ya bidhaa au huduma . udanganyifu wowote ni kosa .
                            
 
                            
                            - 
                                 09
                                Mtandao wa G-Konekti  unamilikiwa na GREDO COMPANY LTD . Hivyo utakuwa unapata taarifa mbalimbali kupitia ujumbe wa maandishi kutoka GREDO.
                            
 
                            
                            - 
                                 10
                                Mtandao wa G-Konekti umesajiliwa, ni salama na una haki miliki zote , Hivyo hupaswi kunakili chochote kwa matumizi binafsi bila ruhusa ya  wamiliki.