Ili kurejesha akaunti yako ya G-konekti, tafadhali jaza taarifa zote kwa usahihi katika fomu iliyopo katika ukurasa huu.
Tafadhali jaza taarifa zako katika fomu hii kama zilivyo katika akaunti yako ya G-Konekti.
SERA, VIGEZO NA MASHARTI
Tafadhali, Soma na Uelewe Vizuri Vigezo, Masharti na Sera za Utumiaji Sahihi Pamoja na Usalama wa Mtandao wa G-Konekti.
01
Chochote unachoweka kutangaza kupitia G-Konekti hakitakiwi kuwa na muonekano au maudhui ya kudhalilisha , kubagua wala yanayokinzana na maadili ya Kiafrika.
02
Tangazo lako baada ya kulipiwa halitawekwa mtandaoni moja kwa moja ,bali litafanyiwa ukaguzi {Review} ndani ya masaa 24, na kama litakidhi vigezo litawekwa mtandaoni , na kama litakuwa halijakidhi vigezo utapewa taarifa ya kutolewa.
03
Ukikiuka vigezo na masharti kwa kuweka picha au maudhui yeyote yasiyofaa kwenye akaunti yako utapewa adhabu ya kuzuiwa kutumia akaunti yako katika kipindi kati ya mwezi mmoja na miaka 3 na endapo baada ya adhabu ukafanya tena kosa lilelile au linalofanana na lile basi utafungiwa akaunti yako na kutoruhusiwa kutumia G-Konekti.
04
Endapo unapata changamoto yeyote ya utumiaji wa G-Konekti wasiliana na wahudumu wetu muda wote.
05
Ili kuvutia watu kuona na kununua bidhaa au huduma yako jitahidi kuweka picha zenye mvuto, zilizopigwa kwa ustadi.
06
Mtandao wetu wa G-Konekti hauruhusu matumizi ya lugha za matusi au lugha za kibaguzi na maudhi.
07
Mpendwa mtumiaji wa G-Konekti mtandao wetu ni salama sana kwa kuwakutanisha muuzaji na mnunuzi wa bidhaa /Huduma .
TAFADHARI; Jiridhishe usalama na ubora wa bidhaa/Huduma kabla ya kununua. G-Konekti haitahusika na utapeli wowote utakaofanyika baina ya muuzaji na mnunuzi nje ya mfumo wetu wa G-Konekti.
08
Mpendwa unaetangaza bidhaa/Huduma yako tafadhari weka taarifa sahihi za muuzaji na hali ya bidhaa au huduma . udanganyifu wowote ni kosa .
09
Mtandao wa G-Konekti unamilikiwa na GREDO COMPANY LTD . Hivyo utakuwa unapata taarifa mbalimbali kupitia ujumbe wa maandishi kutoka GREDO.
10
Mtandao wa G-Konekti umesajiliwa, ni salama na una haki miliki zote , Hivyo hupaswi kunakili chochote kwa matumizi binafsi bila ruhusa ya wamiliki.
Usalama na usiri wa taarifa za mtumiaji yeyote wa G-Konekti ni muhimu kwetu. Hivyo, sera hii ya faragha inaonesha aina ya taarifa ambazo G-Konekti inazikusanya na kuzitumia, namna inavyo zitumia, zisambaza, na kuzihifadhi.
Kwa kutumia G-Konekti, unakubaliana na mwongozo wa faragha ya taarifa za mtumiaji kama ifuatavyo: